Gari moja lenye mabomu lililipuka katika wilaya ya Baghdad mpya, kusini mashariki mwa mji huo, na kusababisha vifo vya watu wanne na wengine wanane kujeruhiwa. Mlipuko mwengine uliotokea kwenye eneo la Al-Madain ambao uliua watu wanne, akiwemo kiongozi mmoja wa kundi la wanamgambo la Sahwa linaloungwa mkono na serikali ya nchi hiyo. Habari kutoka polisi ya Baghdad zinasema, wengi wa watu waliouawa na kujeruhiwa wanatoka wilaya ambazo zina waislamu wengi wa dhehebu la shia. Iraq imeshuhudia mashambulizi mengi zaidi ya kimabavu katika miaka mitano iliyopita, hali ambayo imeongeza hofu kwa umma kuwa matukio hayo ya kimabavu yanaweza kuirejesha nchi hiyo katika migogoro mikubwa ya wenyewe kwa wenyewe iliyotokea mwaka 2006 na 2007, ambapo idadi ya vifo vya watu ilizidi elfu tatu kwa kila mwezi.
20 Julai 2013 - 19:30
Msimbo wa Habari: 443362
Watu 32 wameuawa na wengine 96 kujeruhiwa katika mashambulizi ya mabomu yaliyotegwa kwenye magari ambayo yalitokea jana jioni huko Baghdad, mji mkuu wa Iraq.